admin@forumcc.or.tz   +255 659 266 326

Latest News & Updates

Kama moja ya shuguli za kichumi zinazoendelea jijini Dar Es Salaam uvuvi umechukua kilomita 112 za urefu wa bahari ya hindi. Sekta hii imetoa ajira kwa vijana na wanawake zaidi. Pia, sekta hii imetoa fursa kwa vijana kuwa wavuvi na baadhi ya wanawake kuwa wachuuzi wa Samaki na mazao yake mbalimbali. Shughuli hizi zimekuwa na tija kwani wananchi wanajipatia kipato. Lakini kuna usemi usemao mgagaa na upwa hali wali mkavu, wakazi hawa wanakiri hawakosi kitu kwenye bahari ya hindi jijini Dar Es Salaam. Ila ndani ya miaka kumi na nane iliyopita, mpaka sasa usemi huo wa kiswahili umekosa ukweli kutoka na changamoto mbalimbali ambazo zinahusishwa na mabadiliko ya Tabia nchi.

Disemba 26 2004, uwanda wa Afrika mashiriki ulipatwa na sunami ambayo inakadiriwa kuwa ya tatu kwa ukubwa ndani ya miaka 100. Madhara yalikuwa makubwa, vifo vingi pamoja na unaharibu wa makazi. Ni miaka 18 sasa tokea janga hilo kutokea, lakini Bwana Hujeje Mamboleo anahusisha sunami hiyo kuwa ni sehemu ya sababu ya upungufu wa Samaki. Akiongezea na uvuvi harumu unafanywa na baadhi ya watu, ongezeko la wavuvi na vitendea kazi hafifu vya kufanyia kazi inapelekea kuleta matokeo hasi. “Mimi nimeaanza shuguli zangu za uvuvi mwaka 1978, na kwa kipindi chote tumekuwa tukivua samaki kwa kiasi cha kukidhi biashara zetu.” Bwana Hujeje anaelezea. Anaongezea kuwa kwa miaka yote aliishi msasani ndipo anapofanyia shuguli zake za uvuvi. Lakini baada ya sunami ndipo mabadiliko yalipo aanza. Kwa kipindi cha miaka ya nyuma kuvua kilo 100 hadi kilo 500 ilikuwa ni kitu cha kawaida sana.

Bwana Hujeje ambaye pia ni katibu wa chama cha wavuvi wadogo wadogo msasani amekari kuwepo na ukataji wa miti ya mikoko kwa ajili ya utengeneazeaji wa mitubwi. Hivyo kuathiri mazalia ya Samaki, lakini mmomonyoko wa fukwe za bahari kwani mikoko ndio miti pekee huweza kukuwa katika ardhi ya chumvi na kutunza fukwe za bahari. Akaongezea pia, “ unajua pia mikoko ndio miti pekee ambayo huvuta hewa ya kaboni dioskidi kwa wingi Zaidi? Ukataji unaharibu mazingira hivyo kuongeza hewa ya kaboni dioskidi angani” Kwa miaka yake yote ya uvuvi anaelezea juu ya majira ya uvivu yaliyokuwepo. Kila majira na kina cha maji kulikuwa na aina na idadi mahususi ya Samaki. Lakini kwa sasa ni tofauti, kupata Samaki ni bahati sio kwa majira. “Sisi na wakulima tulikuwa tuna lugha zinazoendana, ukiona embe zimezaliwa nyingi basi huo mwaka Samaki watakuwa adimu”. Aneelezea kuhusu uhusiano wa kilimo na uvuvi. “kwa sasa hakuna haja kutumia aina za majira tulizo tumia zamani kwani hazifanyi kazi, Samaki hawapo tena”. Swali ni nini hali imekuwa hivi? Samaki wameendea wapi?

Kama Bwana Hujeje alivyoelezea ongezeko la wavuvi eneo moja limekuwa sababu yao wavuvi kupata Samaki wachache. Linaweza kuwa sababu ambayo iko moja kwa moja, lakini hakuna uzalishaji wa Samaki ambao utakuwa toshelevu kwa wote? Ni mambo madogo ambayo yanaweza kuonekana hayana tija kwa sasa na kupuuziwa ila ndio chanzo kikubwa cha uharibifu. Sababu zinaweza kuwa nyingi na nyingine nyingi kuongezewa. Ni muda wa kukiri kuwa mabadiliko ya tabia nchi yamesabishwa na sababu ndogo ndogo ambazo tumeona na kama maisha ya kawaida. Lakini matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi leo yanahusishwa na sababu zingine kama vile ukosefu wa vifaa, si kweli.

Samaki wanaweza kuzaliwa kwa wingi kama mazalia yao yakitunza vizuri na kukomesha uvuvi haramu. Kutenga sehemu ambazo ni za kuvulia Samaki pia kuzipumzisha mara kwa mara. Ongezeko la watu ni jambo moja, lakini watu kuwepo na katika shuguli moja ya uchumi sio jambo sahihi. Vijana wapanue mawazo na kujishugulisha na shuguli zingine za uchumi kama vile kilimo. Alisisitiza Mzee Hujeje Aliendelea kwa kuelezea kuwa, zipo baadhi ya jitihada ambazo tumekwishaaanza kuzifanya ikiwa ni pamoja na upandaji wa mikoko katika fukwe.

Akihitimisha maelezo yake, Mzee Hujeje alitoa Rai kuwa wanaiomba Serikari, Asasi zisizo za kiserikali na wadau wote wa maendeleo kutoa elimu kwa wavuvi juu ya ukataji holela wa miti, kutoa elimu juu ya fursa zingine tofauti na uvuvi ili kupunguza watu kutegemea uvuvi tu kama sehemu ya kuingizia kipato chao.

 

It is a non-for-profit, member-based - of over 80 diverse organizations across Tanzania committed to work on climate change issues in Tanzania and beyond.

Web Traffic

1611603
Today
This Week
This Month
All days
48
3012
17502
1611603

Get In Touch

P O Box 123
Salasala-Magwaza Street
Dar es Salaam, Tanzania

+255 659 266 326

admin@forumcc.or.tz